DKT. MARRY MWANJELWA AFUNGUA WARSHA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO

Na. Halima Katala Mbozi.

Chuo cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kipo tayari kushirikiana na Serikali katika  kutekeleza sera mbalimbali za kilimo nchini ili kufanikisha lengo la Tanzania ya Viwanda.


Akizungumza na wanahabari katika Warsha ya kupokea Ripoti ya takwimu ya  matokeo ya  mbegu bora  makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha SUA Prof. Raphael Chibunda amesema wao kama chuo cha kilimo wapo tayari kushirikiana na Serikali  katika kupamabana na kutekeleza Sera za kilimo bora nchini kwa kupitia tafiti mbalimbali zinazofanywa chuoni hapo.

 “Sisi kama Chuo cha Kilimo kwa kupitia tafiti zetu tunazofanya chuoni kwetu tunaahidi kushirikiana na serikali kupitia wizara ya kilimo katika kutekeleza Sera za kilimo nchini”. Amesema Chibunda

 MAKAMU MKUU WA CHUO CHA SOKOINE CHA KILIMO SUA AKIZUNGUMZA KATIKA UFUNGUZI WA WARSHA YA KUWASILISHA MATOKEO YA UTAFITI NA MAPENDEKEZO YA UBORESHAJI SERA KATIKA SEKTA YA KILIMO MKOANI MOROGORO.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa kilimo Mhe. Merry Mwanjelwa amesema watu waache kufanya kazi kimazoea badala yake wafanye kazi kwa ufanisi na utaalamu Zaidi ili kuleta matokeo makubwa ya tafiti zinazofanyika kwa lengo la kuhamasisha jamii kiujumla.


NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE. DKT MARRY MWANJELWA AKIFUNGUA WARSHA YA KUWASILISHA MATOKEO YA UTAFITI NA MAPENDEKEZO YA UBORESHAJI SERA KATIKA SEKTA YA KILIMO MKOANI MOROGORO.
Naye Bi. Veronika Soko  Mwakilishi wa  MVIWATA  kutoka Mbeya ambaye ni mkulima mdogo amesema wakulima wengi bado wamekuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na mbegu bora hasa zinazotolewa na wataalamu hivyo kuwataka wataalamu wawe wanatoa elimu Zaidi kwa wakulima wengi badala ya kuita wachahe.

KUSHOTO NI MWAKILISHI WA KATIBU TAWALA MKOA ERNEST MKONGO,  KULIA NI RASI WA NDAKI YA SHULE KUU YA UCHUMI KILIMO NA STADI ZA BIASHARA DR. ADAM M. AKYOO WAKIFUATILIA UFUNGUZI WA WARSHA YA KUWASILISHA MATOKEO YA UTAFITI NA MAPENDEKEZO YA UBORESHAJI SERA KATIKA SEKTA YA KILIMO MKOANI MOROGORO.
“ukiangalia jambo ambalo tunalijadili leo limewakilishwa na wakulima  watatu kutoka nyanda za juu, kusini na nyanda za kati kwamba hao ndo wakulima huku wengi wakiwa ni maafisa kilimo wa wilaya ambapo  wakulima wengi hawana uelewa na elimu ya kutoka kuhusu hizo pembejeo hivyo unakuta taarifa nyingi haziwafikii  kutokana na kutofika moja kwa moja kwa wahusika wenyewe”.

Comments

Popular posts from this blog

PISHI LA LEO: JUISI YA UBUYU NA MAAJABU YAKE KATIKA TIBA