Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake ya kuwepo hapa juu ya ardhi. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu. Tukianza na unga wa ubuyu huu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi zaidi ya matunda mengine yoyote unayoyafahamu. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa. Aidha, pia ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) zaidi ya kile ambacho hupatikana katika maziwa ya ng’ombe, hali kadhalika madini mengine ambayo hupatikana katika ubuyu ni madini ya chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo nayo hupatikana kwa kiwango kingi zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi. Ubuyu pia husaidia kujenga neva za fahamu mwilini na ina virutubisho vya kulinda mwili na kuongeza kinga ya mwili hii ni kutokana na k...